Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 05:23

Raia wa Ghana wanapiga kura kumchagua rais na wabunge


Upigaji kura Ghana 2020 ukiendelea kwa njia ya kielektroniki
Upigaji kura Ghana 2020 ukiendelea kwa njia ya kielektroniki

Kinyang’anyiro kinatazamwa kati ya Rais aliyepo madarakani Nana Akufo-Addo wa chama cha New Patriot na rais wa zamani John Mahama kiongozi wa chama cha upinzani cha National Democratic Congress

Upigaji kura umeanza Ghana huko Afrika magharibi kumchagua rais na wajumbe wa bunge lenye viti 275.

Japokuwa kuna wagombea 12 wanaowania kiti cha urais, kinyang’anyiro kinatazamwa kua kati ya Rais aliyepo madarakani Nana Akufo-Addo wa chama cha New Patriot na rais wa zamani John Mahama kiongozi wa chama cha upinzani cha National Democratic Congress.

Hiki ni kinyang’anyiro cha tatu kati ya viongozi hawa wawili tangu mwaka 2012, wakati Mahama alipomshinda Akufo Addo, ikifuatiwa na ushindi wa Akufo Addo mwaka 2016. Wakati huo huo wanawake watatu ni miongoni mwa wagombea 11 wanaompa changamoto Akufo-Addo, lakini macho yameeelkezwa kwa Jane Naana Opoku-Agyeman, waziri wa zamani wa elimu ambaye ni mgombea mwenza wa Makamu Rais wa Mahama akiwa mwanamke wa kwanza kusimama kwa tiketi ya chama kikubwa cha kisiasa nchini Ghana.

Chombo cha Habari chenye makao makuu yake Congo cha Africa News, kilinukuu utafiti wa karibuni uliofanywa na Center for Democratic Development unaonesha kwamba Akufo-Addo anaongoza kwa idadi ndogo dhidi ya Mahama.

XS
SM
MD
LG