Viongozi wa wanafunzi waliandamana na raia wa Bangladesh leo Jumamosi kwa kampeni ya kitaifa ya kutotii ya kiraia wakati serikali ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina ikikabiliwa na hali mbaya zaidi ya ukandamizaji unaofanywa na polisi unaosababisha vifo kwa waandamanaji.
Maandamano dhidi ya ajira kwenye huduma za umma yalisababisha siku kadhaa za ghasia mwezi uliopita na yaliua zaidi ya watu 200 katika baadhi ya ghasia mbaya zaidi za miaka 15 ya utawala wa Hasina.
Vikosi vya jeshi vilivyopelekwa kwa muda mfupi vilirejesha tena hali ya utulivu, lakini umati wa watu uliingia mitaani kwa idadi kubwa baada ya sala ya Ijumaa katika taifa hilo lenye Waislamu wengi, wakiitikia wito wa viongozi wa wanafunzi kuishinikiza serikali ili kupatikana muafaka zaidi.
Forum