Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 13:35

Raia 12, askari wapoteza maisha shambulizi la California


Polisi wakiwa wamelizingira eneo ambako shambulizi la bunduki lilitokea huko California Jumatano usiku, Novemba 11, 2018.
Polisi wakiwa wamelizingira eneo ambako shambulizi la bunduki lilitokea huko California Jumatano usiku, Novemba 11, 2018.

Watu 12 ikiwa ni pamoja na polisi mmoja wameuawa baada ya mtu mwenye bunduki kuingia katika baa California Kusini nchini marekani na kuanza kufyatua risasi Jumatano usiku.

Kulingana na Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Ventura, Geoff Dean, mshambuliaji huyo pia ameuawa ingawa haikufahamika mara moja aliuawa na nani.

Watu wengine kadha wamejeruhiwa katika shambulizi hilo katika kitongoji cha Thousand Oaks nje kidogo ya mji wa los angeles. Miongoni mwa waliouawa ni pamoja na polisi wa siku nyingi aliyekuwa kazini kwa miaka 29, sajenti ron helus.

"Sajenti helus amekufa…. Baada ya kufikishwa hospitali. Nasema tu inaweza kuwa ugaidi kwa sababu huko ndiko tunakoenda siku hizi likitokea tukio kama hili. Hakuna sababu yoyote tunayoifahamu mpaka sasa katika mauaji haya mabaya. Sina lolote linalofanya nidhanie hivyo, au FBI, kwamba ni ugaidi, lakini bila shaka tunaangalia hilo pia," ameeleza mkuu wa polisi.

Maelezo kuhusu shambulizi hilo yamekuwa yakitofautiana huku ripoti za awali zikisema mshambuliaji amekamatwa, lakini Sheriff Dean amehakikisha kuwa mshambuliaji aliuwawa.

Mashahidi waliliambia shirika la utangazaji la CNN kuwa baa hiyo ilikuwa imejaa vijana – wengi wa vyuo vikuu – kwa ajili ya kunywa na kucheza densi.

Risasi zilipoanza kuvuma baadhi ya watu walivunja madirisha kwa kutumia viti katika jitahada za kutoka.

Moja wa manusura amesema : Risasi zilianza kuvuma. Tulijificha chini ya viti na kulikuwa na bomu dogo la moshi. Rafiki yangu aliona bomu hilo la moshi likianza kutoa moshi, na mara tukasikia kila mtu akisema “kimbia” tukakimbia nje hadi kwenye eneo la kuegeshea magari.

Baadhi ya mashahidi na watu wengine waliandika katika mitandao ya kijamii kuwa mshambuliaji huyo huenda alifyatua risasi zaidi ya 30. Maafisa wanasema shambulizi lilikuwa likiendelea wakati maafisa wa kwanza walipowasili katika eneo la tukio.

XS
SM
MD
LG