Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:50

Radio BBC yaruhusiwa kutangaza tena nchini Burundi.


Makao makuu ya BBC mjini London, Julai 19, 2017. Picha ya AP.
Makao makuu ya BBC mjini London, Julai 19, 2017. Picha ya AP.

Mamlaka inayosimamia vyombo vya habari nchini Burundi Jumatano imetangaza kwamba imeondoa marufuku ya kuikataza radio BBC kupeperusha matangazo yake kote nchini, miaka mitatu baada ya radio hiyo ya Uingereza kulazimika kusitisha matangazo yake katika taifa hilo la Afrika mashariki.

Baraza la kitaifa la kufuatilia utangazaji habari ( CNC) lilifuta leseni ya BBC mwaka wa 2019, likishtumu radio hiyo kukiuka sheria ya vyombo vya habari na kutofuata maadili ya utangazaji habari.

“Tumefikia uamuzi wa kuifungua tena radio BBC kuanzia leo,” mwenyekiti wa CNC Vestine Nahimana amesema.

Idhaa hiyo ilikidhi masharti yaliyowekwa na serikali, ameongeza.

Sauti ya America pamoja na BBC zote zilisimamishwa mwezi Mei mwaka wa 2018.

Idhaa hizo mbili zilisimamishwa wiki mbili kabla ya kura ya maoni ya kufanyia marekebisho katiba, ili kumruhusu rais wa zamani Pierre Nkurunziza kuongoza hadi mwaka wa 2034.

XS
SM
MD
LG