Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:00

Jumba la maonyesho la Smithsonian Marekani, kufanya onyesho la kwanza kuu la Quran


Qurani ya zama iliopo katika chuo kikuu cha Birmingham Uingereza.
Qurani ya zama iliopo katika chuo kikuu cha Birmingham Uingereza.

Kitabu cha Quran, inayoheshimiwa na waislamu, ni kivutio kikuu katika maonyesho hapa Marekani wakati jumba la makumbusho la Smithsonian, linaonyesha waraka kutoka mojawapo ya mkusanyiko mkubwa wa maandishi ya Quran.

Ukumbi wa Arthur M Sackler kwenye jumba la maonyesho la Smithsonian ulitangaza Jumanne kuwa maonyesho ya : The Art of the Quran: Treasures from the museum of Turkish and Islamic Arts”, yaani Sanaa ya Quran: Hazina kutoka makumbusho ya sanaa za Kituruki na Kiislamu”, italeta pamoja waraka 48 na maandishi kutoka jumba la maonyesho la Istanbul pamoja na mkusanyiko wa maandishi kutoka ukumbi wa sanaa wa Sacler and Freer, ambao kwa pamoja ni maonyesho ya Smithsonian ya sanaa ya Kiasia.

Maonyesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa Oktoba 15, wiki kadhaa kabla ya uchaguzi wa rais, na yataendelea hadi Februari 20, 2017.

Dini ya kiislam na Quran ni masuala ambayo huwenda yakaibuka sana wakati wa midahalo na majadiliano, lakini Massumeh Farrhad , mkuu wa maonyesho ya sanaa ya kiislamu katika ukumbi wa Sacler na Freer anasema maonyesho hayo ni nafasi ya kuwasilisha riwaya tofauti, anasema hii ni nafasi ya kulenga umuhimu wa kitabu cha Quran kama kazi za sanaa na umuhimu wake katika historia.

Maandishi ya kiarabu katika Quran yaliandikwa katika karne ya 7, lakini aina za Quran zilizopo ni jambo la kushangaza.

Qurani hizi za awali zilitokea mashariki ya kati, Misri, Syria, Afghanistan, Iran , Uturuki na Iraq.

Maonyesho haya ni nafasi kwa watu wa Marekani kuziona Quran hizi kwa karibu zaidi na kuzingatia juu ya dhana zao.

XS
SM
MD
LG