Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 13, 2024 Local time: 09:30

Qatar inawasihi Israel na Hamas kujitolea kusitisha mapigano


Qatar ni mpatanishi muhimu katika vita vinavyoendelea huko Gaza kati ya israel na Hamas.
Qatar ni mpatanishi muhimu katika vita vinavyoendelea huko Gaza kati ya israel na Hamas.

Hayo yanajiri wakati Israel bado ikiahidi kuuvamia mji wa kusini wa Rafah licha ya wasiwasi wa ulimwengu kwa maelfu ya Wa-palestina.  

Afisa mwandamizi wa Qatar amewasihi wote Israel na Hamas kuonyesha “kujitolea zaidi na umakini mkubwa” katika mashauriano ya kusitisha mapigano kwenye mahojiano na vyombo vya habari vya Israel wakati shinikizo likiongezeka kwa pande zote mbili kuelekea katika makubaliano ambayo yatafanya mateka wa Israel kuwa huru na kuleta uwezekano wa kusitisha vita vya takribani miezi saba huko Gaza.

Mahojiano na gazeti litolewalo kila siku la Haaretz na shirika la utangazaji la Israel Kan, yalichapishwa na kurushwa Jumamosi jioni. Hayo yanajiri wakati Israel bado ikiahidi kuuvamia mji wa kusini kabisa wa Rafah licha ya wasiwasi wa ulimwengu kwa maelfu ya Wa-palestina wanaojihifadhi katika eneo hilo na huku pande hizo zikibadilishana mapendekezo kuhusiana makubaliano ya kusitisha mapigano.

Qatar, ambayo ni mwenyeji wa makao makuu ya Hamas mjini Doha imekuwa mpatanishi muhimu katika vita vya Israel na Hamas. Pamoja na Marekani na Misri, Qatar ilikuwa muhimu katika kusaidia mashauriano ya sitisho la muda la mapigano mwezi Novemba ambalo lilipelekea kuachiliwa kwa darzeni ya mateka.

Forum

XS
SM
MD
LG