Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:57

Putin aweka marufuku ya uuzaji wa mafuta ya Russia kwa nchi za magharibi


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Rais wa Russia Vladimir Putin Jumanne amesaini amri ambayo inaweka marufuku ya uuzaji wa mafuta na bidhaa za mafuta kwa mataifa yaliyoweka kikomo cha bei ya mafuta ya Russia, kuanzia Februari 1 kwa kipindi cha miezi mitano.

Kundi la G7 la nchi tajiri duniani, Umoja wa Ulaya na Australia walikubaliana mwezi huu kikomo cha dola 60 kwa pipa moja la mafuta ghafi ya Russia, hatua ambayo ilianza kutekelezwa Disemba 5 kwa sababu ya “operesheni maalum ya kijeshi” ya Moscow nchini Ukraine.

Amri hiyo ya Kremlin ilieleza “Hatua hii inaanza kutekelezwa Februari 1, 2023, na inaendelea hadi Julai 1, 2023.”

XS
SM
MD
LG