Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:13

Putin awapatia fursa wapiganaji wa Wagner kuendelea kuhudumu pamoja nchini Russia


Rais wa Russia, Vladimir Putin akiwa mjini Moscow. July 10, 2023. (Photo by Alexander Kazakov / SPUTNIK / AFP)

Putin alihojiwa  na gazeti la kila siku la Russia la Kommersant alisema hii ilikuwa ni moja ya ofa kadhaa alizotoa katika mkutano wake na wapiganaji wapatao darzeni tatu  na mwanzilishi wa Wagner, Yevgeny Prigozhin, mwishoni mwa mwezi uliopita, siku tano baada ya Wagner kufanya uasi

Rais wa Russia Vladimir Putin aliwapatia wapiganaji mamluki wa kundi la Wagner fursa ya kuendelea kuhudumu pamoja nchini Russia baada ya uasi wao, alisema katika mahojiano yaliyochapishwa Alhamisi jioni.

Putin alihojiwa na gazeti la kila siku la Russia, la Kommersant, alisema hii ilikuwa ni moja ya ofa kadhaa alizotoa katika mkutano wake na wapiganaji wapatao darzeni tatu na mwanzilishi wa Wagner, Yevgeny Prigozhin, mwishoni mwa mwezi uliopita, siku tano baada ya Wagner kufanya uasi ambao haukufanikiwa dhidi ya uongozi wa kijeshi wa Russia.

Chini ya makubaliano hayo, wapiganaji hao wangekuwa chini ya kamanda wao wa sasa, ambaye gazeti hilo lilimtaja tu kwa kutambulisha kuwa ni “Grey Hair.” Putin pia alisema ni juu ya serikali ya Russia na bunge kushughulikia muundo wa kisheria kwa ajili ya kuunda jeshi binafsi.

Kommersant ilisema Putin alizungumza juu ya kukutana na wapiganaji 35 wa Wagner na Prigozhin huko Kremlin na kuwapa njia mbadala kwa siku zijazo, ikiwa ni pamoja na kubaki chini ya kamanda wao kwa miezi 16.

Forum

XS
SM
MD
LG