Katika matamshi yake ya ufunguzi, Putin aliesema, ”Kuimarika kwa ushirikiano kati ya mataifa yetu kunaendelea vyema kwenye nyanja zote, zikiwemo kiuchumi, kijamii, kitamaduni, kielimu na hata kijeshi ." Kremlim ilirusha video fupi iliyomuonyesha Putin akisalimiana na Li na kisha kuketi kwenye meza moja.
Waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu pia alikuwepo kwenye kikao hicho. Wiki iliyopita Beijing ilitangaza kuhusu ziara ya Li nchini Russia akisema kwamba angekutana na maafisa wa ulinzi , bila kutaja kwamba angekutana na Putin. Rais wa China Xi Jinping mwezi uliopita pia alikutana na Putin mjini Moscow.