Ikiwa imebaki miezi miwili kabla ya kuingia mwaka wa pili tangu uvamizi kamili wa Russia nchini Ukraine, Putin amesisitiza kwamba Russia inalenga kuhakikisha kumalizwa kwa misimamo ya ki Nazi, kuondolewa kwa silaha, pamoja na msimamo usioegemea upande wowote wa Ukraine, wakati alipokuwa akiongea na wana habari ikiwa ni mkutano wake wa mwisho wa mwaka.
Russia imerejea kusema kwamba serikali ya Ukraine ina ushawishi mkubwa wa makundi yenye misimamo mikali yakiwemo ya Nazi, madai ambayo Ukraine na washirika wake wa magharibi wameyapuuza na kusema hayana msingi kufanya uvamizi. Putin pia amesema kwamba Ukraine kamwe isijunge na NATO. Muungano huo hata hivyo umerudia mara kadhaa kusema kwamba ni jukumu la mataifa binafsi na siyo Russia.
Forum