Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:29

Putin asema kwamba hataongeza wapiganaji zaidi nchini Ukraine


Rais wa Russa Vladimir Putin akiwa kwenye kikao cha baraza la kitaifa la haki za binadamu mjini Moscow, Dec. 7, 2022.
Rais wa Russa Vladimir Putin akiwa kwenye kikao cha baraza la kitaifa la haki za binadamu mjini Moscow, Dec. 7, 2022.

Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatano amesema kwamba huenda vita vya Ukraine vikachukua muda mrefu, lakini haoni haja ya kuongeza wanajeshi wengine kwenye uwanja wa vita.

Putin wakati akiwa kwenye kikao na baraza la haki za binadamu la Kremlin linalojumuisha wanahabari , wanaharakati na maafisa wa umma, amesema kwamba Russia itaendelea kujilinda kwa namna yoyote ile kwenye vita vya Ukraine.

Putin wakati wa mkutano huo uliyorushwa kwa njia ya televisheni alisema kwamba Russia inaonekana na mataifa ya Magharibi kama isiyo na dhamana yoyote ya kuendelea kuwepo.

Septemba na Oktoba, Putin alituma wapiganaji 300,000 wa ziada nchini Ukraine, hatua iliyoshangaza wakazi wengi wa taifa hilo. Hatua hiyo pia ilipelekea maelfu ya wanaume wa Russia kutoroka nchini wakihofia kutumwa kwenye uwanja wa vita.

XS
SM
MD
LG