Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:46

Dawa mpya yaweza kuzuia uambukizaji Ukimwi kwa wanawake


Bango katika mkutano wa Vienna
Bango katika mkutano wa Vienna

Watafiti watangaza dawa mpya inayoweza kuzuia uambukizaji virusi vya HIV kwa wanawake katika mkutano wa kimataifa wa ukimwi.

Watafiti wa Afrika Kusini wametangaza maendeleo makubwa katika kupambana na ukimwi baada ya kugundua dawa ya kupaka ambayo inaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa uambukizaji wa virusi vya HIV kwa wanawake. Watafiti wanasema dawa hiyo inaweza kuwa kinga kubwa kwa wanawake, na kuwawezesha kujilinda dhidi ya wapenzi wao wanaokataa kutumia mipira ya kondom.

Tangu kuanza kwa ugonjwa wa ukimwi karibu miaka 30 iliyopita, wanasayansi wamekuwa wakitafiti aina fulani ya dawa au kinga inayoweza kutumiwa katika sehemu za siri za mwanamke kujikinga na uambukizaji wa virusi vya HIV.

Sasa, wanasayansi wawili wa Afrika Kusini ambao wanafanya kazi na Kituo cha Utafiti wa Ukimwi Afrika Kusini (CAPRISA) wanasema majaribio ya dawa hiyo ya kupaka iliyoshirikisha wanawake 889 Afrika Kusini imeonyesha mafanikio. Dawa hiyo ya kupaka ambayo ina kemikali aina ya tenofovir.

Hata hivyo, wataalam wanatahadharisha kwamba uchunguzi zaidi unahitajika kuhakikisha dawa hiyo ni salama na inafanya kazi kabla ya kuanza kutolewa kwa matumizi ya umma.

XS
SM
MD
LG