Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 15:26

Ureno yafuta ukame wa magoli


Cristiano Ronaldo akimruka kipa wa Korea kaskazini na kupachika bao la 7.

Ureno imeivunja vunja Korea Kaskazini kwa jumla mabao 7-0 huko Capetown Afrika Kusini

Ureno imeivunja vunja Korea Kaskazini kwa jumla mabao 7-0 huko Capetown Afrika Kusini na kushika nafasi ya pili katika Kundi G.

Wakicheza kwenye mvua isiyopungua Raul Meireles alifunga bao kunako dakika ya 29 ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Lakini katika kipindi cha pili safu ya ushambuliaji ya Ureno ilizidi kuwaka moto na kupachika magoli sita zaidi.

Wafungaji wa magoli hayo kwa Ureno ni Simao Sabrosa,Hugo Almeida, Liedson, Tiago (2) na Christian Ronaldo .
Na katika kundi H Chile waliifunga Uswiss kwa taabu bao 1-0 huku timu hiyo ikiwa na wachezaji 10 baada ya mchezaji wao machachari Behrami kupewa kadi nyekundu.

Winga wa zamani wa Liverpool Mark Gonzalez aliipatia nchi yake bao la ushindi kwa kichwa baada ya dakika 67 za ukuta mkali wa Switzerland wakiwa na wachezaji 10 tu na kuweka rekodi ya kuwa timu iliyolinda lango lake kwa muda mrefu zaidi kuliko nyingine mpaka hivi sasa kwenye kombe la dunia.

Nao timu ya Spain hatimaye ilipata ushindi wake wa kwanza baada ya kuibwaga Honduras mabao 2-0.

Alikuwa ni David Villa aliyepachika mabao yote mawili kiufundi kunako dakika ya 17 na 51.

Mchezaji huyu hatari pia alikosa penati katika dakika ya 62. Spain wana nafsi kubwa ya kuingia kwenye raundi ya pili ambapo kundi lao litategemea zaidi na magoli lakini wana nafasi ya kuongoza kundi hili kama wakishinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Chile.


XS
SM
MD
LG