Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:58

Papa Francis awasili Marekani


Papa Francis, kushoto, akikaribishwa na Rais Barack Obama na mkewe Michelle Obama.
Papa Francis, kushoto, akikaribishwa na Rais Barack Obama na mkewe Michelle Obama.

Huku kukiwa na kiwingu kwa mbali Papa Francis aliwasili Washington mchana katika uwanja wa ndege wa kituo cha kijeshi cha Andrews, nje kidogo ya Washington, kuanza ziara yake ya kwanza na ya kihistoria Marekani.

Ndege ya Papa Francis inayoitwa "Shepherd 1" iligusa ardhi ya Marekani saa tisa na dakika 49 kwa saa za Washington, nje kidogo ya mji huu. Alikaribishwa na kundi la makadinali sita - wote wakiwa katika mavazi yao meusi. Mamia ya waumini na watu wengine walifika uwanjani hapo kumkaribisha.

Rais Obama amkaribisha Papa Francis
Rais Obama amkaribisha Papa Francis

Washington ni kituo cha kwanza cha ziara yake ya siku tano nchini Marekani baada ya kumaliza ziara ya siku nne nchini Cuba. Kiongozi huyo wa kanisa katoliki alikuwa kiungo kikubwa katika mazungumzo ya kurejesha uhusiano kati ya Cuba na Marekani.

Kutoka uwanja wa ndege wa kijeshi wa Andrews Papa Francis alingia katika msafara wa magari hadi katika ubalozi wa Vatican, Washington, ambako atalala.

Ziara ya Papa Francis Marekani
Ziara ya Papa Francis Marekani

Akiwa hapa Marekani Papa Francis atakutana na Rais Obama katika White House Jumatano na baadaye kufanya misa kubwa katika kanisa la Basilica ambayo inatazamiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya elfu 25.

Kutoka Washington atakwenda New York na baadaye pia kutembelea mji wa Philadelphia.

XS
SM
MD
LG