Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:39

Polisi yaendelea na msako mkali dhidi ya al- Shabab Kenya

Wapiganaji wa al- Sabab wanavyoonekana katika picha
Wapiganaji wa al- Sabab wanavyoonekana katika picha

Polisi ijumaa walisema madaktari walikamatwa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi na walitakiwa kufikishwa mahakamani ijumaa kwa makosa yanayohusiana ugaidi.

Polisi nchini Kenya inaendelea na msako mkali na imewakamata madaktari wawili wanaotuhumiwa kuhusika na kundi la wanamgambo la al-Shabab wakati jeshi la nchi hiyo linaendelea kuwatafuta wanamgambo wa al- Sahabab katika mpaka wake na Somalia.

Polisi ijumaa walisema madaktari walikamatwa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi na walitakiwa kufikishwa mahakamani ijumaa kwa makosa yanayohusiana ugaidi.

Mashambulizi ya ardhini na ya anga yanalenga maeneo ya kundi hilo linalojihusisha na al- Qaida kusini mwa Somalia. Maafisa wa jeshi wanasema wamechukua udhibiti wa mji wa mwambao wa Somalia wa Ras Kamboni na wanasema wako karibu na Kismayo kituo muhimu cha al- Shabab.

Kenya inalaumu al- Shabab kwa kuwateka raia wa kigeni katika ardhi ya Kenya tuhuma ambazo kundi hilo limekanusha.

Wakati huo huo katika mji mkuu wa Mogadishu, kundi la al-Sabab linaonekana kuteka wilaya nyingi baada ya mapambano dhidi yake na jumuiya ya umoja wa afrika.

XS
SM
MD
LG