Vikosi maalum vya polisi vilifyatua gesi ya kutoa machozi kwa wapiganaji hao, ambao polisi wamesema ni makundi yanayounga mkono na yanayoipinga serikali ya Eritrea, yanayohudhuria mkutano mjini The Hague.
Polisi na kikosi cha zimamoto zimesema wakati wa ghasia hizo, mawe, fataki na vitu vingine vilirushiwa, ambapo baadhi yao walikuwa na silaha za kupigia watu. Watu hao waliteketeza magari mawili ya polisi na basi la watalii.
Wakati wa fujo hizo, maafisa wawili walipata majeraha mikononi mwao na mwingine kwenye meno yake. Wa nne aligongwa na gari la polisi katika ghasia hizo.
Polisi imekamata watu kadhaa na wameita mashahidi na kutumia picha za video kwa ajili ya uchunguzi ghasia hizo unaoendelea.
Forum