Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:53

Polisi wakanusha kumzuilia meya wa Kampala


Meya wa Kampala Erias Lukwago (kulia) nje ya mahakama ya Buganda.
Meya wa Kampala Erias Lukwago (kulia) nje ya mahakama ya Buganda.
Polisi wa Uganda wamekanusha vikali ripoti kuwa wanamzuilia meya wa Kampala anayekabiliwa na utata Erias Lukwago na kwamba wameizuia familia yake kumpelekea Chakula na madawa.

Msemaji wa Polisi mjini Kampala Ibin Ssenkunbi anasema maafisa wa ulinzi walipata taarifa za kijasusi kuwa bw. Lukwago alikuwa anapanga wafuasi wake kuyumbisha usalama mjini humo kwa kuzusha ghasia katika ofisi za mamlaka ya Kampala KCCA.

Ssenkunbi aliiambia sauti ya Amerika kuwa meya Lukwago alikuwa ametangaza mpango kwa watu kuungana naye kuzivamia ofisi za mamlaka ya mji wa Kampala KCCA na kwa hiyo polisi wakaonelea wachukue hatua kuzia ghasia mjini humo.

Matamshi ya msemeji huyo wapolisi yalifuatia agizo la spika wa bunge la Uganda, kwa inspekta mkuu wa polisi kuhakikisha kuwa meya Lukwago na familia yake wanapata chakula na madawa bila kuvurugwa. Baadhi ya wabunge walimwomba spika kuingilia kati mzozo unaomkabili meya huyo, wakisema polisi wamemzuilia nyumbani kwake na kwamba mke wake aliyejifungua wiki mbili zilizopita amezuiwa pia kutafuta huduma za matibabu.

Lakini Ssenkunbi anakanusha madai hayo, akisema kuwa mawakili wa meya huyo wameruhusiwa kumwona ikiwa ni pamoja na familia yake na marafiki zake. Anasema maafisa wa polisi wanafuata sheria kwa mujibu wa katiba ya Uganda kuhakikisha ulinzi wa raia na kwa hivyo hawataruhusu mtu au watu kuvuruga amani na kutumbukiza mji wa Kampala katika ghasia.
XS
SM
MD
LG