Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 07:34

Polisi wafunga magazeti mawili ya Uganda


Polisi wasimkama zamu nje ya ofisi za gazeti la Daily Monitor mjini Kampala Mei 20, 2013
Polisi wasimkama zamu nje ya ofisi za gazeti la Daily Monitor mjini Kampala Mei 20, 2013
Polisi wa Uganda walivamia ofisi za gazeti la Daily Monitor mchana wa Jumatatu na kuwaeleza wakuu wa gazeti hilo kwamba eneo hilo limefungwa kwa uchunguzi wa uhalifu wakiwa wanatafuta barua.
Mahojiano na Joseph Odondo - 5:30
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:30 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akizungumza na Sauti ya Amerika mkurugenzi wa uhariri wa Daily Monitor Joseph Ddindo, anasema wameambiwa na maafisa wa polisi walovamia ofisi zao kwamba "wanatafuta barua ambayo wanaamini maripoti wetu walikuwa nayo ambayo ndiyo msingi wa ripoti moja tulochapisha wiki iliyopita".

Anasema barua hiyo ilihusika na Jenerali David Tinyefuza mkuu wa idara za ujasusi ambapo alimomba mkurugenzi wa idara ya ujasusi wa ndani kufanya uchunguzi katiika mtuhuma za njama ya kutaka kuwauwa maafisa wakuu wa jeshi na siasa wanaonekana kupinga mpango wa Rais Yoweri Museveni kumkabidhi madaraka kijana wake anapostahafu.
XS
SM
MD
LG