Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 09:23

Polisi waendelea kumsaka mtu aliyeua kwa risasi watu 18 katika jimbo la Maine


Picha ya Robert Card, mshukiwa wa mauaji ya watu 18 katika mji wa Lewiston, ilitolewa na polisi wa mji huo, Oktoba 25, 2023
Picha ya Robert Card, mshukiwa wa mauaji ya watu 18 katika mji wa Lewiston, ilitolewa na polisi wa mji huo, Oktoba 25, 2023

Mamia ya polisi na maafisa wengine wa usalama wameendelea na msako mkali leo Ijumaa katika jimbo la Marekani la Maine wakimtafuta mtu ambaye mamlaka inamuhusisha na mauaji ya watu 18 kwa kuwapiga risasi kwenye eneo la mchezo wa Bowling na kwenye baa katika mji mdogo wa Lewiston.

Mkuu wa polisi katika jimbo la Maine Kanali William Ross amesema mshukiwa Robert Card, anapaswa kuchukuliwa kuwa mtu mwenye silaha na hatari” na kwamba watu wowote wanaoweza kukutana naye wanapaswa kuwaita polisi badala ya kukabiliana naye.

Polisi na maafisa wengine wa usalama Alhamisi walionekana kwa uingi kwenye nyumba iliyoko Lewiston ya ndugu wa Card.

Shule za umma za Lewiston na shule za wilaya karibu na Lewiston zemefungwa leo Ijumaa wakati mamlaka zinaendelea na msako wao.

Forum

XS
SM
MD
LG