Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 08:13

Polisi wa Uganda wathibitisha kumshikilia mwandishi mwengine wa vitabu.


Polisi wa Uganda wakipiga doria kwenye barabara moja mjini Kampala. Novemba 19, 2020. Picha ya AP.
Polisi wa Uganda wakipiga doria kwenye barabara moja mjini Kampala. Novemba 19, 2020. Picha ya AP.

Mwandishi wa vitabu na mwanaharakati wa Uganda Norman Tumuhimbise ni miongoni mwa wanahabari tisa waliokamatwa kutokana na mawasiliano ya kuudhi, polisi walisema Jumatatu.

Ni mwandishi wa vitabu wa pili kukamatwa na maafisa katika miezi ya karibuni.

Tumuhimbise ambaye anaongoza kundi la shinikizo la ndani ya nchi, The Alternative Movement na chombo cha habari cha mtandaoni, Alternative Digital, alikuwa anatarajiwa kuzindua kitabu cha kumkosoa rais Yoweri Museveni tarehe 30 Machi.

Inasemekana Tumuhimbise na wenzake walikamatwa na kuwekwa ndani ya gari na maafisa wa usalama waliokuwa na silaha Alhamisi iliyopita.

Msemaji wa polisi, Fred Enanga ameliambia shirika la habari la AFP kwamba “ Polisi walipata malalamiko kuwa kundi hilo lilihusika katika mawasiliano ya kuudhi na kutangaza matamshi ya chuki”.

Wakili wa washukiwa hao, Eron Kiiza aliiomba mahakama ya mjini Kampala iwaachilie huru jana Jumatatu, akidai kuwa polisi walichukuwa simu, laptop, kinasa sauti na kamera za chombo cha habari cha Tumuhimbise.

XS
SM
MD
LG