Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 16:47

Polisi huko Uganda Wamezuia Maandamano ya Leo, Alhamis


Polisi wa Uganda
Polisi wa Uganda

Polisi wa Uganda wamepiga marufuku maandamano yaliyopangwa Alhamis wakati wabunge wakijadili mipango wa kuondoa umri wa rais kuhudumu ikionekana kama juhudi ya kufungua njia kwa Yoweri Museveni kuwania muhula wa sita kama kiongozi wa nchi hiyo.

Wabunge wa chama tawala wanatarajiwa kusonga mbele na muswaada wa kufanya marekebisho katika kipengele cha katiba kinachoelezea rais lazima awe na umri wa miaka kati ya 35 hadi 75. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 anasema ana miaka 73 ambapo kwa sheria ya sasa hastahili kuwania tena uongozi katika uchaguzi wa mwaka 2021. Hata hivyo umri wake halisi bado ni suala ambalo linajadiliwa sana.

Jenerali Kale Kayihura, mkuu wa polisi Uganda
Jenerali Kale Kayihura, mkuu wa polisi Uganda

Mkuu wa polisi nchini Uganda Kale Kayihura alisema katika taarifa yake kwamba maandamano yaliyopangwa yalilenga kusababisha ghasia na vurugu na hivyo aliwasihi waandamanaji kufanya mikutano ndani ya majengo ili kutoa maoni yao.

XS
SM
MD
LG