Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:19

Polisi wa Tanzania wamkamata mshukiwa wa bomu la Nairobi


Mlipuko kwenye jengo la biashaa kati kati ya Nairobi Mai 28.
Mlipuko kwenye jengo la biashaa kati kati ya Nairobi Mai 28.

Polisi wa Tanzania wanamshikilia mtuhumiwa anaeaminika ni Emrah Erdogan anaetafutwa na polisi wa Kenya na Uganda

Polisi nchini Tanzania imesema Jumanne kuwa imemkamata mshukiwa mkuu wa ugaidi raia wa Ujerumani ambaye alikuwa akitafutwa na polisi wa Kenya kufuatia mlipuko mmoja wa bomu katika mji mkuu wa Nairobi uliotokea mwezi uliopita na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Polisi wa Kenya mwezi uliopita walitoa picha ya mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Emrah Erdogan raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki ambaye anajulikana pia kama Salahuddin al-Kurdi. Polisi wa Kenya walisema aliingia nchini humo akitokea Somalia mwezi Mei.

Vyombo vya habari vya Ujerumani vinaeleza kwamba Erdogan alisafiri kuelekea kaskazini-mashariki ya Waziristan nchini Pakistan mwanzoni mwa mwaka 2010 na kujiunga na kundi la wanamgambo wa ki-Islam. Kisha alikwenda Somalia mwaka 2011 na alishukiwa kujiunga na kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye uhusiano na al-Qaida.

Mshukiwa huyo raia wa Ujerumani yupo kizuizini jijini Dar-Es-Salaam, Tanzania kwa mashtaka yanayohusiana na uchunguzi wa ugaidi.

XS
SM
MD
LG