Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:43

Polisi wa Kenya wazuia shambulizi la kigaidi


Polisi wa Kenya wakiimarisha usalama katika sehemu za mikusanyiko
Polisi wa Kenya wakiimarisha usalama katika sehemu za mikusanyiko

Polisi nchini Kenya Jumanne waliwakamata watu watatu waliogundulika wakiwa na bomu la kienyeji walipoingia kwenye eneo la maduka ya kifahari. Shirika la habari la Ufaransa-AFP limeripoti.

Kwa mujibu wa idara ya polisi ya Kenya bomu hilo liliteguliwa kwa usalama na kulidhibiti lisilipuke.

AFP lilimkariri mkuu wa polisi, bwana Robinson Mboloi ambaye anaongoza kituo cha polisi cha Kasarani katika mji mkuu Nairobi akisema kuwa wamewatia mbaroni wanaume watatu ambao waligundulika kuwa na bomu hilo la kienyeji na kitufe cha kulilipua. Eneo la maduka ambalo wanaume hao walikamatwa ni la Garden City Mall.

Bwana Mboloi alisema maafisa wa kitengo kinachoshughulika na milipuko walitegua bomu hilo na eneo hilo la maduka liko salama.

Eneo hilo la maduka ambalo liko mjini Nairobi lilifunguliwa mapema mwaka huu, na kuelezewa kuwa kituo kikubwa cha maduka ya kifahari katika Afrika mashariki.

Kenya imekumbwa na mlolongo wa mashambulizi yaliyofanywa na waasi wenye uhusiano na kundi la wanamgambo wa kisomali la Al-shabaab ambao miaka miwili iliyopita walishambulia eneo la maduka la kifahari la Westgate Mall.

Westgate Mall ni miongoni mwa majengo yaliyoshambuliwa
Westgate Mall ni miongoni mwa majengo yaliyoshambuliwa

Katika shambulizi hilo wanamgambo hao wa kiislamu walivamia na kuua watu takriban 67 na wafanyakazi katika siku nne za ghasia wakidai ni majibu kwa jeshi la Kenya kuwepo nchini Somalia.

Wanaume watatu waliokamatwa Jumanne wameripotiwa kuwa wote ni wakenya na walisimamishwa wakiwa pamoja na maafisa usalama kwenye eneo la ukaguzi la kuingia kwenye kituo cha maduka.

Mboloi alisema kitufe cha kutegua bomu kilionekana wakati wa ukaguzi na shukran kwa kazi nzuri ya wana usalama. Na kuongezea watachunguzwa ili kufahamu mahusiano yao na ugaidi wa kundi la Al-shabaab.

Tangu mashambulizi ya Westgate, kundi la Al-shabaab limeendelea kuishambulia Kenya ndani ya ardhi yake huku shambulizi kubwa zaidi likiwa ni lile la mwezi April mwaka huu wakati washambuliaji wanne wa kujitoa mhanga walipowaua watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa kilichopo kaskazini mashariki mwa Kenya, wengi wao wakiwa wanafunzi.

XS
SM
MD
LG