Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 00:14

Polisi wa Afrika Kusini wawakamata watu 20 wanaoshukiwa kuchochea ghasia mbaya mwaka jana


Watu wasimama karibu na nyumba zao wakiwatizama wanajeshi wa Afrika Kusini wakishika doria katika eneo lao katika kitongoji cha Alexandria, Johannesburg, Julai 15, 2021. Picha ya AFP
Watu wasimama karibu na nyumba zao wakiwatizama wanajeshi wa Afrika Kusini wakishika doria katika eneo lao katika kitongoji cha Alexandria, Johannesburg, Julai 15, 2021. Picha ya AFP

Polisi wa Afrika Kusini Alhamisi wamesema wamewakamata watu 20 wanaoshukiwa kuwa miongoni mwa watu waliochochea vurugu ambazo zilisababisha vifo vya mamia ya watu mwaka jana, katika mzozo mbaya kuwahi kutokea tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi.

.Maafisa wamesema timu za pamoja za polisi zilihamasishwa kuteketeza ukamataji wa wakati mmoja katika mikoa mbalimbali.

Kukamatwa kwa watu hao kunajiri wakati wapelelezi walipiga hatua kubwa kwa kuchunguza uchochezi wa ghasia kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa mengine wakati wa wimbi la machafuko mwezi Julai 2021, polisi wamesema katika taarifa.

Baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini yalitumbukia katika machafuko na zaidi ya watu 350 waliuawa katika kipindi cha siku 10 za ghasia zilizofuatia kufungwa kwa rais wa zamani Jacob Zuma mwezi Julai mwaka jana.

Polisi wamesema washukiwa hao 20 waliokamatwa walitarajiwa kufika mbele ya mahakama ya Durban leo Ijumaa kusikiliza mashtaka yanayowakabili, kuanzia njama ya kufanya ghasia hadi uchochezi wa kuchoma moto.

XS
SM
MD
LG