Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:12

Polisi Ugiriki wamewakamata wasafirishaji wa biashara haramu


Ramani ya Ugiriki na nchi jirani nazo
Ramani ya Ugiriki na nchi jirani nazo

Washukiwa hao sita, ni raia mmoja wa Syria, mmoja wa Palestina na raia wanne wa Iraq, walikamatwa Jumamosi katika kijiji kilicho umbali wa kilomita 10 kutoka mpaka wa Albania, polisi wamesema Jumapili. Wanachama wengine saba wa genge hilo walikamatwa katika eneo hilo-hilo Septemba 28

Polisi nchini Ugiriki wamewakamata watu sita ambao wanasema ni wanachama wa genge kubwa la biashara ya usafrishaji wa binadamu ambalo lilipora fedha kutoka kwa wahamiaji ili kuwasaidia kuvuka mpaka na kuingia katika nchi jirani ya Albania na kusafiri kwenda nchi za Umoja wa Ulaya kuelekea kaskazini.

Washukiwa hao sita, ni raia mmoja wa Syria, mmoja wa Palestina na raia wanne wa Iraq, walikamatwa Jumamosi katika kijiji kilicho umbali wa kilomita 10 kutoka mpaka wa Albania, polisi wamesema Jumapili. Wanachama wengine saba wa genge hilo walikamatwa katika eneo hilo-hilo Septemba 28.

Wakati huo huo wahamiaji 11 walipatikana wamefungwa pingu na walitelekezwa kwenye kituo cha jeshi. Polisi walisema mwezi Septemba kwamba wasafirishaji ambao tayari walikuwa wamekusanya zaidi ya euro 1,000 (takribani dola 1,100) kutoka kwa kila kichwa cha mhamiaji ili kuwasaidia kuvuka kuingia Albania, waliwakamata wakidai euro 1,500 zaidi.

Polisi wamesema wasafirishaji waliwatesa wahamiaji hao, walirekodi video za mateso na kutuma picha hizo kwa ndugu wa waathirika katika Mashariki ya Kati na Asia Kusini.

Forum

XS
SM
MD
LG