Polisi nchini Bangladesh wamewakamata karibu viongozi 8,000 wa upinzani katika msako wa nchi nzima tangu maafisa wa polisi walipovunja mkutano mkubwa wa hadhara kwenye mji mkuu wiki moja iliyopita, ripoti imesema Jumapili.
Wimbi kubwa la watu kukamatwa linakuja kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Januari. Chama kikuu cha upinzani nchini humo, Bangladesh Nationalist Party (BNP), na washirika wake wamekuwa wakifanya maandamano makubwa katika miezi ya hivi karibuni wakimtaka Waziri Mkuu Sheikh Hasina ajiuzulu na kuruhusu serikali isiyoegemea upande wowote kusimamia uchaguzi huo.
Hasina amesimamia ukuaji mzuri katika miaka yake 15 ya uongozi, lakini anashutumiwa kwa kulitawala taifa hilo la Asia Kusini kwa mabavu. Marekani imewawekea vikwazo baadhi ya maafisa wake waandamizi wa polisi kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.
Zaidi ya wafuasi 100,000 wa upinzani walijiunga na maandamano katikati mwa Dhaka Jumamosi iliyopita, wakati polisi mmoja alipouawa katika mapambano. Tangu wakati huo polisi wameanzisha msako mkali dhidi ya BNP, na kuwakamata maelfu ya wanaharakati na kuwatuhumu angalau viongozi wake 162 wa nafasi ya juu kwa mauaji ya afisa huyo.
Forum