Washukiwa wanamgambo wanaotaka kujitenga wamewaua polisi wanne wa Nigeria na raia wawili wakati wa mapambano ya bunduki walipokuwa wakifanya doria kusini mashariki mwa nchi hiyo polisi imesema Jumamosi.
Shambulio la mapema Ijumaa asubuhi lilifanyika katika eneo la Ngor-Okpala katika Jimbo la Imo mahala ambako kundi la wazawa wa Biafra (IPOB) wanaotaka kujitenga na kitengo chake cha silaha Eastern Security Network (ESN) bado wanaendesha harakati zao.
Mashambulizi yanayolaumiwa kwa IPOB yamesababisha vifo vya maafisa kadhaa wa polisi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita katika majimbo ya kusini- mashariki mwa Nigeria ambako kundi hilo linawasumbua watu wa kabila la Igbo. IPOB mara kwa mara imekanusha kuhusika na mashambulizi dhidi ya polisi, ofisi za serikali za mitaa na majengo ya taasisi za uchaguzi.
Kujitenga ni suala nyeti nchini Nigeria ambako tangazo la Jamhuri huru ya Biafra lililotolewa na maafisa wa jeshi la Igbo, kusini -mashariki mwa nchi hiyo mwaka 1967 lilisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitatu ambavyo vilisababisha vifo vya zaidi ya watu milioni moja.