Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 02:01

Polisi DRC wazuia kuapishwa Tshisekedi


Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi DRC
Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi DRC

Eneo linaloelekea nyumbani kwa Tshisekedi mtaa wa Limete nalo limezingirwa na polisi

Polisi mjini Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefyatua mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi waliokusanyika karibu na uwanja wa mashujaa kwa sherehe za kuapishwa kiongozi huyo kama rais, siku tatu baada ya rais Kabila kuapishwa kwa awamu ya pili.

Haijafahamika mpaka sasa kama Tshisekedi ataweza kufika katika uwanja huo, hatua ambao wafuatiliaji wanasema itazusha machafuko mjini humo. Polisi wamezingira barabara nyingi katika eneo la Limete mjini Kinshasa anakoishi kiongozi huyo wa upinzani.

Kiasi cha wafuasi wapatao 1,000 wa Tshisekedi walikusanyika karibu na uwanja wa Mashujaa mapema leo asubuhi, lakini vifaru kadha ya jeshi la Congo navyo vilikuwa karibu.

Saa kadha baada ya saa ambayo sherehe hizo zilipangwa kufanyika, msemaji wa Tshisekedi alisema bado alikuwa nyumbani na alikuwa anashauriana na wenzake kuhusu hatua ya kuchukua.

Mkuu wa polisi Charles Bisengimana alisema hali ya Kinshasa ni shwari. Alisema hajua kama Tshisekedi ataweza kuendelea na mipango yake hiyo ya kuapishwa Ijumaa.

XS
SM
MD
LG