Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:55

Polisi 30 wauwawa kaskazini mwa Kenya


بھارتی ریاست اتر پردیش میں رواں ہفتے ’لٹھ مار ہولی‘ کا ایک انوکھا تہوار منایا گیا۔
بھارتی ریاست اتر پردیش میں رواں ہفتے ’لٹھ مار ہولی‘ کا ایک انوکھا تہوار منایا گیا۔
Watu wenye silaha huko kaskazini mwa Kenya wamewauwa maafisa polisi wasiopungua 30 ambao walikuwa wakiwasaka wezi wa mifugo.

Polisi nchini Kenya wanasema maafisa hao walishambuliwa ghafla jumamosi wakati gari lao lilipokuwa likielekea kwenye eneo moja la kaskazini katika wilaya ya Baragoi.

Timu za uchunguzi na uokozi ziligundua miili 11 siku ya jumamosi na miili 19 mingine siku iliyofuata. Watu tisa walionusurika na shambulizi hilo wamelazwa hospitali.

Hakuna mtu yeyote aliyedai kuhusika na shambulizi hilo. Polisi wanashuku wezi wa mifugo walihusika na shambulizi jingine huko Baragoi mwezi uliopita ambalo liliuwa watu 13.

Wizi wa mifugo na ghasia zinazohusiana na hilo zinatokea mara kwa mara huko kaskazini mwa Kenya lakini mashambulizi ya moja kwa moja kwa polisi ni nadra sana.

Maafisa wa serikali walisema wameshtushwa na mauaji hayo na walielezea wasi wasi kuhusu maandalizi na uwezo wa majeshi ya usalama.
XS
SM
MD
LG