Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 02:49

Polisi 13 wa Sudan wauwawa huko Darfur.


Walinda amani wa Umiojja wa mataifa wakifanya doria huko el Fasher Sudan.
Walinda amani wa Umiojja wa mataifa wakifanya doria huko el Fasher Sudan.

Polisi 13 wameuwawa na wengine 30 kujeruhiwa katika jaribio la kuokoa mateka huko Darfur.

Maafisa wa usalama nchini Sudan wanasema maafisa wa polisi 13 wameuwawa na wengine wasiopungua 30 wamejeruhiwa wakati wa jaribio la kuokoa mateka katika mkoa tetea wa Darfur jana alhamisi.

Polisi wanasema maafisa hao walijaribu kuwaokoa wanajeshi watatu huko Jebel Mara wakati walipokabiliwa na genge la watu wenye silaha. Gazeti moja la Sudan la al-Ahdath linasema mateka mmoja ni mfanyakazi wa kutoa msaada raia wa Italy, aliyetekwa nyara mwezi uliopita.

Lakini afisa wa usalama huko Darfur aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba mtu huyo hakuhusika katika tukio hili. Tangu mapigano yaanze kati ya waasi na majeshi ya serikali huko Darfur miaka minane iliyopita, inakadiriwa watu laki tatu wameuwawa na takribani watu milioni 3 wengine wamezikimbia nyumba zao.

XS
SM
MD
LG