Maafisa wa polisi nchini Kenya wameripotiwa kuuwa watu watatu na kujeruhi wengine kadhaa Jumatano jioni katika eneo la Bondo Kaunti ya Siaya ilioko magharibi mwa nchi wakati walipokuwa wakiandamana wakiwa na nia ya kushambulia wanawake wawili wa umri wa makamu walioshukiwa kufanya biashara haramu ya kuuza watoto.
Utumiaji wa risasi kutoka kwa polisi wakati wa kutawanya maandamano hayo hata hivyo ulikemewa vikali na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu. Katika siku za hivi kariuni, maafisa wa usalama nchini humo wamekuwa wakilaumiwa kwa kutumia risasi za moto wakati wa kutawanya maandamano kama anavyoeleza mwandishi wa VOA Kennedy Wandera kutoka Nairobi.
Bonyeza kwa taarifa zaidi.