Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:47

Polisi wa Kenya na Uganda wachunguza mlipuko wa Nairobi

Mbwa maalumu wa polisi akinusa mizigo nje ya basi lililohusika na ajali ya mlipuko wa bomu mjini Nairobi, Dec 20,2010
Mbwa maalumu wa polisi akinusa mizigo nje ya basi lililohusika na ajali ya mlipuko wa bomu mjini Nairobi, Dec 20,2010

Polisi nchini Uganda na Kenya wanachunguza uwezekano kwamba magaidi wenye kushirikiana na al-Qaida huenda wanahusika kwa mlipuko mmoja wa bomu uliowauwa watu kadhaa mjini Nairobi.

Polisi nchini Uganda na Kenya wanachunguza uwezekano kwamba magaidi wenye kushirikiana na al-Qaida huenda wanahusika kwa mlipuko mmoja wa bomu uliowauwa watu kadhaa mjini Nairobi.

Bomu hilo lililipuka Jumatatu jioni karibu na basi moja la abiria lililokuwa likisafiri kutoka Nairobi kuelekea Kampala, na kumuua mtu mmoja aliyeaminika kusafirisha mlipuko huo. Hakuna yeyote aliyedai kuhusika na mlipuko huo ambao uliwajeruhi zaidi ya watu 40.

Afisa polisi wa cheo cha juu wa Uganda, Kale Kayihura, alisema Jumanne kuwa anaamini wanamgambo wa al-Shabab kutoka nchini Somalia walihusika na mlipuko. Al-Shabab walidai kuhusika na shambulizi moja la bomu lililotokea mwezi Julai mjini Kampala ambalo liliuwa watu 76.

Maafisa wa Kenya wanachunguza kama bomu hilo linahusiana na mashambulizi mawili ya maguruneti ya hivi karibuni mjini Nairobi ambayo yaliwaua maafisa polisi watatu wa Kenya.

Wote maafisa wa Kenya na Uganda wanasema wanaongeza ulinzi kufuatia tukio hilo.

XS
SM
MD
LG