Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 17:09

Nyumba ya Kamishna wa Polisi yashambuliwa Zanzibar


Polisi washika doria kwenye barabara za Zanzibar kwenye picha ya awali.
Polisi washika doria kwenye barabara za Zanzibar kwenye picha ya awali.

Watu wasio julikana, usiku wa kuamkia Jumanne walishambulia nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi la Zanzibar kwa kutumia kile kinachoaminika kuwa bomu.

Wakati Vikosi vya ulinzi na usalama vikiendelea kuimarisha hali ya amani na utulivu visiwani Zanzibar, watu wasiojulikana wanadaiwa kurusha kitu kinachodhaniwa kuwa bomu na kulipua kwenye paa la nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi, Zanzibar Bw Hamdan Omar Makame, usiku wa kuamkia Jumanne katika eneo la Kijichi lililoko nje kidogo ya jiji la Zanzibar.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:24 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kamishna Hamdan amesema kuwa shambulizi hilo lilitokea mwendo wa saa tano usiku akiongeza kuwa jeshi lake kamwe halitaruhusu vitendo vya uvunjivu wa Sheria hasa wakati huu kisiwa hicho kinachojiandaa kwa uchaguzi wa marudio. Amesema kuwa uchunguzi umeanza na ana uhakika kuwa waliotekeleza shambulizi hilo watatiwa nguvuni.

XS
SM
MD
LG