Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 20:13

Pistorius afutiwa mashtaka makubwa ya mauaji


Wanafamilia wa mwanamitindo Reeva Steenkamp, wakisikiliza taarifa ya jaji Masipa, Sept. 12, 2014.
Wanafamilia wa mwanamitindo Reeva Steenkamp, wakisikiliza taarifa ya jaji Masipa, Sept. 12, 2014.

Mwanariadha maarufu nchini Afrika kusini, Oscar Pistorius amekutwa na hatia ya kusababisha kifo cha mpenzi wake Reeva Steenkamp, lakini alifutiwa mashtaka makubwa ya mauaji ya mpenzi wake huyo wa kike.

Jaji Thokozile Masipa alisoma uwamuzi hapo Ijumaa kwa kesi iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu dhidi ya mwanariadha huyo aliyeshiriki katika mashindano ya Olympic, anayejulikana kama “The Blade Runner” ambaye alimpiga risasi na kumuuwa mwanamitindo Reeva Steenkamp akiwa nyumbani kwa Pistorius, tukio lililotokea Februari mwaka 2013.

Pistorius mwenye umri wa miaka 27 hakuonesha hisia wakati jaji alipokuwa akisoma mashtaka hayo. Waendesha mashtaka walitoa hoja kwamba Pistorius alitenda tukio hilo kwa makusudi wakati alipomfyatulia risasi Steenkamp kupitia mlango wa bafuni uliokuwa umefungwa ndani ya nyumba yake Pistoria katika eneo la Pretoria, nchini Afrika kusini.

Pistoria alisema alidhani alikuwa akimfyatulia risasi mwizi aliyeingia usiku ndani ya nyumba yake.

XS
SM
MD
LG