Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 20:34

Pence: Nakubaliana na Uamuzi wa Rais Trump Kumlazimisha Flynn Kujiuzulu


Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg (Kulia) akimkaribisha Makamu wa Rais Mike Pence makao mkuu ya NATO, Brussels, Belgium, Feb. 20, 2017.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg (Kulia) akimkaribisha Makamu wa Rais Mike Pence makao mkuu ya NATO, Brussels, Belgium, Feb. 20, 2017.

Makamu wa Rais Mike Pence amesema "alisikitishwa” na alichokifanya aliyekuwa Mshauri wa Usalama wa Taifa Michael Flynn baada ya kujua amemficha taarifa muhimu.

Pence amesisitiza kuwa anakubaliana na uamuzi wa Rais Donald Trump kumtaka Flynn ajiuzulu wiki iliyopita kutokana na kumpotosha.

Makamu wa Rais aliulizwa suala hili linalo husu taarifa alizotoa Flynn kwake, wakati wa mkutano na waandishi katika makao makuu ya NATO Jumatatu.

Kwa sababu hiyo Rais Trump akamtaka Flynn, jenerali mstaafu kujiuzulu kwa kumficha Pence kuhusu mazungumzo yake ya simu na balozi wa Russia Washington kabla ya uongozi mpya kuchukua madaraka, White House imesema.

Mkuu wa wafanyakazi wa Trump amesema mtu atayeteuliwa katika wadhifa huo wa mshauri wa usalama atakuwa na amri juu ya kuamua nani afanye kazi katika Baraza la Usalama la Taifa (NSC).

Suala hili juu ya nani mwenye mamlaka katika kuchagua wafanyakazi wa NSC ni moja ya sababu ya mstaafu Admirali wa jeshi la majini Robert Harward kukataa kuchukua nafasi hiyo wiki iliyopita.

“Rais Trump ameweka wazi kwamba mkurugenzi mpya wa NSC atakuwa na madaraka kamili ya kuunda Baraza lake na vitengo vyote vya NSC,” mkuu wa wafanyakazi wa White House, Reince Priebus ameiambia FOX News Jumapili.

Haward alikuwa chaguo la kwanza la Trump kuchukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Flynn, ambaye aliondolewa katika wadhifa huo baada ya kutumikia kwa siku 24.

XS
SM
MD
LG