Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:36

Paul Ryan ndie spika mpya wa Marekani


Paul Ryan akizungumza muda mfupi baada ya kuchaguliwa kuwa spika, Oct. 29, 2015.
Paul Ryan akizungumza muda mfupi baada ya kuchaguliwa kuwa spika, Oct. 29, 2015.

Mbunge wa jimbo la Wisconsin, m-conservative machachari Paul Ryan alichaguliwa Alhamis kama spika mpya katika baraza la wawakilishi la Marekani.

Kwenye upigaji kura uliofanyika zaidi katika misingi ya chama dhidi ya upinzani wa Democrat, wa-Republican walio wengi katika bunge walimchagua Ryan mwenye umri wa miaka 45 kuchukua wadhifa wa juu katika bunge.

Kama spika wa bunge, anakuwa mmoja wa wanasiasa wenye nguvu mjini Washington na mtu wa pili katika kurithi urais. Ryan amemrithi John Boehner, mbunge wa jimbo la Ohio ambaye anaondoka bungeni baada ya kutumikia miaka 25 ambapo miaka mitano ya mwisho alihudumu kama spika wa bunge.

John Boehner, akibubujikwa na machozi bungeni, October 29, 2015.
John Boehner, akibubujikwa na machozi bungeni, October 29, 2015.

Katika hotuba ya kuaga iliyomtoa machozi, Boehner alisema anastaafu, bila kujuta na wala mzigo, na kutoa fursa kwa sera mbali mbali na mpango mpya wa matumizi ya serikali katika kipindi hiki.

XS
SM
MD
LG