Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 20:34

Papa kutoa hotuba kwenye bunge Uingereza


Papa Benedict yuko Uingereza katika siku ya pili ya ziara yake ya kihistoria ya siku nne.

Papa Benedict yuko Uingereza katika siku ya pili ya ziara yake ya kihistoria ya siku nne.

Ratiba yake ya Ijumaa inajumuisha kikao pamoja na Askofu wa Canterbury Rowan William kiongozi wa kanisa la Anglikan, katika ishara ya kuonyesha umoja kati ya makanisa hayo yaliyogawanyika.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki pia atatoa hotuba mbele ya wabunge katika bunge la Uingereza.

Papa Benedict alianza ziara yake Alhamisi kwa kukiri kwamba viongozi wa kanisa wameshindwa kuwa makini na wameshindwa kupambana haraka na tabia ya baadhi ya mapadri ambao kwa miongo kadhaa wamewalawiti na kuwabaka watoto kwenye parokia zao.

Katika misa iliyofanyika nje huko Glasgow Scotland Papa Benedict aliwahimiza Waingereza kukataa kutojihusisha na dini na kuonya juu ya hatari za kutohusisha imani za dini katika masuala ya umma.

XS
SM
MD
LG