Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:50

Papa Francis Jumanne kuyatembelea  mataifa mawili yalio matatani barani Afrika


Papa Francis katika mkutano wake wa kila wiki mjini Vatican. Mei 25, 2022. REUTERS
Papa Francis katika mkutano wake wa kila wiki mjini Vatican. Mei 25, 2022. REUTERS

Papa Francis Jumanne anaanza ziara ya mataifa mawili dhaifu ya Kiafrika ambayo mara nyingi yamesahauliwa na ulimwengu, ambako mizozo ya muda mrefu imesababisha mamilioni ya wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi wanaokabiliwa na njaa.

Ziara ya Papa kuanzia Januari 31 hadi Februari 5 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sudan Kusini, inampeleka kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani mwenye umri wa miaka 86 hadi sehemu ambazo Wakatoliki ni takriban nusu ya wakazi wao na ambako Kanisa hilo ni mdau muhimu katika afya na mifumo ya elimu pamoja na juhudi za kujenga demokrasia.

Ziara hiyo ilipangwa kufanyika Julai mwaka jana lakini iliahirishwa kwa sababu Francis alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya muda mrefu ya goti. Bado anatumia kiti cha magurudumu na fimbo lakini goti lake limeimarika sana.

Nchi zote mbili zina utajiri mkubwa wa maliasili - DRC katika madini na Sudan Kusini katika mafuta lakini zinakabiliwa na umaskini na migogoro.

DRC, ambayo ni nchi ya pili kwa ukubwa barani Afrika na ina wakazi wapatao milioni 90, inapata ziara yake ya kwanza ya Papa tangu John Paul II alipolitembelea taifa hilo mwaka 1985, wakati ilipokuwa ikijulikana kama Zaire.

XS
SM
MD
LG