Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 23:13

Papa Francis atoa Baraka za Krismas


Papa Francis akibusu sanamu la mtoto Yesu kwenye mkesha wa ibada ya siku ya Krismas huko St. Peter's Basilica, Vatican

Papa Francis ametoa Baraka zake za Krismas kwa mwaka wa pili akiwa madarakani kwa maelfu ya watu waliokusanyika katika eneo la St.Peters Square mahala ambako alitumia fursa ya siku ya Krismass kulaani kile alichokiita mateso mabaya wanayofanyiwa watu wachache na kundi la Islamic State ambalo lilidhibiti maeneo mengi nchini Syria na Iraq mwanzoni mwa mwaka huu.

Christmass ni moja ya siku takatifu kwa wakristo ambao siku ya Alhamis wanasheherekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Papa alizungumzia migogoro mingi mikubwa na matatizo yanayoendelea duniani akisihi Amani katika maeneo kama Ukraine, Nigeria na Jamhuri ya Afrika ya kati na kulaani shambulizi la wiki iliyopita lililofanywa na kundi la Taliban dhidi ya wanafunzi nchini Pakistan.

Papa Francis akiongoza ibada huko Vatican
Papa Francis akiongoza ibada huko Vatican

Papa pia alitoa Baraka kwa waathirika wa ugonjwa wa Ebola hususani watu nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea pamoja na watu wanaotoa huduma za tiba.

Katika siku ya Krismas kwenye mji wa ukingo wa magharibi wa Bethlehem, wakristo walikusanyika kwenye kanisa la Nativity kwa ibada kwenye eneo ambalo wanaamini Yesu alizaliwa.

Mchungaji wa kanisa la Latin Patriarch of Jerusalem, Fouad Twal aliongoza waumini kwenye ibada ya asubuhi kwa saa za huko iliyohudhuriwa na mamia ya watu.

XS
SM
MD
LG