Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 10:03

Papa Francis aomba Israel na Hamas kuweka silaha chini


Kiongozi wa kanisa Katoloki, Papa Francis.
Kiongozi wa kanisa Katoloki, Papa Francis.

Papa Francis Jumapili  ameomba kuwepo sitisho la mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas, na kutoa  wito mwingine wa kuachiliwa kwa watu waliotekwa nyara na kushikiliwa na kundi la wanamgambo wa Palestina huko Gaza.

“Asiwepo yeyote atakaye puuzia wazo la kuweka silaha chini,” amesema wakati wa hotuba yake ya kila wiki kwenye bustani ya St Peters. “Sitisho la mapigano,” alisema, wakati akielezea ombi la karibuni kwa njia ya televisheni lilitolewa na Father Abraham Faltas mmoja wa wawakilishi wa Vatican katika Ardhi Takatifu.

Pia aliongeza maneno kwa maneno yake , “Tunasema sitisho la mapigano, kina kaka na dada, tuache vita. Vita siku zote ni kushindwa tu.” Papa Francis amesema hayo wakati vikosi vya Israel vikifanya mashambulizi ya ardhini dhidi ya wanamgambo wa Hamas huko Gaza, katika kile ambacho waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekiita awamu ya pili ya vita vya wiki tatu ambavyo vimelenga kulitokomeza kundi hilo.

Wakati huo huo ripoti zinasema kwamba maelfu ya wakazi wa Gaza walivamia ghala za shirika la UN kwa wakimbizi wa Palestina, UNRWA, na kuchukua unga pamoja na bidhaa nyingine za msingi, shirika hilo limesema Jumapili.

Forum

XS
SM
MD
LG