Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 15:38

Papa Francis anatoa ombi la haraka kusitishwa kwa mzozo huko Gaza


Papa Francis
Papa Francis

“Ninaendelea kufikiria kuhusu hali mbaya ya wa-Palestina na Israel ambako watu wengi wamepoteza maisha. Ninawaomba kwa jina la Mungu, sitisheni mapigano” alisema, akizungumza na umati wa watu katika uwanja wa St. Peter baada ya sala yake ya kila wiki ya Angelus

Papa Francis leo Jumapili ametoa ombi la haraka la kusitishwa kwa mzozo huko Gaza, akiomba misaada ya kibinadamu na msaada kwa wale waliojeruhiwa ili kupunguza hali mbaya sana ya kibinadamu”.

“Ninaendelea kufikiria kuhusu hali mbaya ya wa-Palestina na Israel ambako watu wengi wamepoteza maisha. Ninawaomba kwa jina la Mungu, sitisheni mapigano” alisema, akizungumza na umati wa watu katika uwanja wa St. Peter baada ya sala yake ya kila wiki ya Angelus.

“Ni matumaini yangu kuwa yote yatafanyika ili kuepusha mzozo huo kuongezeka, kwamba majeruhi wataokolewa na misaada itafika kwa watu wa Gaza, ambako hali ya kibinadamu ni mbaya sana,” alisema.

Papa Francis amerudia wito wake wa sitisho la mapigano na kuachiliwa huru kwa mateka waliochukuliwa na Hamas wakati wa shambulio lake la Oktoba 7, akiwalenga watoto, ambao alisema “lazima warudi kwenye familia zao”.

“Tuwafikirie watoto, watoto wote waliohusika katika vita hivi, kama vile Ukraine na katika migogoro mingine, mustakbali wao unauliwa”, aliongeza.

Papa Francis mwenye umri wa miaka 86 tayari ametoa wito wa kuanzishwa kwa njia za kibinadamu na amesema suluhisho la mataifa mawili linahitajika ili kumaliza vita vya Israel na Hamas.

Forum

XS
SM
MD
LG