Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:13

Papa Francis anatarajiwa kuwasili DRC na Sudan Kusini siku ya Jumanne


Papa Francis akiwa kwenye kiti cha magurudumu huko Vatican. 31 Mei, 2022.
Papa Francis akiwa kwenye kiti cha magurudumu huko Vatican. 31 Mei, 2022.

Papa anatembelea  nchi hizo mbili ambako miaka mingi ya mizozo imewalemaza wengi na bado ni miongoni mwa maeneo magumu zaidi duniani kupata upatikanaji na uelewa. Ziara yake inawatia moyo Wakatoliki na wasio Wakatoliki pia

Papa Francis anatarajiwa kuwasili Congo na Sudan Kusini wiki ijayo, ambako maelfu ya watu watamuangalia kwa mbali amekaa kwenye kiti chake cha magurudumu na kuendesha harakati zote ikizingatia ishara maalum ya msalaba.

Papa huyo ambaye alianza kutumia kiti cha magurudumu mwaka jana anazitembelea nchi hizo mbili ambako miaka mingi ya mizozo imewalemaza wengi na bado ni miongoni mwa maeneo magumu zaidi duniani kupata upatikanaji na uelewa. Ziara yake inawatia moyo Wakatoliki na wasio Wakatoliki pia.

"Tunajua kwamba ni mateso, lakini pia inatufariji kuona mtu mkubwa kama Papa akitumia kiti cha magurudumu," alisema Paul Mitemberezi, mchuuzi wa sokoni mjini Goma, kiini cha eneo la mashariki mwa Congo linalotishiwa na makundi kadhaa yenye silaha. "Wakati mwingine inatupa ujasiri wa matumaini kwamba huu sio mwisho wa dunia na mtu anaweza kuishi."

Mitemberezi, Mkatoliki na baba, amekuwa mlemavu tangu akiwa na umri wa miaka 3 kwa sababu ya ugonjwa wa polio. Anafanya kazi kuisaidia familia yake kwa sababu hawezi kufikiria maisha ya kuomba-omba. Akiwa njiani kuelekea sokoni, kiti chake cha magurudumu matatu kinaharibiwa kwa mawe yaliyopo barabara yanayokwamisha safari yake.

XS
SM
MD
LG