Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 17:10

Papa Francis amekutana na wakimbizi na watu maskini huko Hungary


Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis

Papa Francis alitumia fursa hiyo kuwakumbusha  "waamini wajibu wao wa Kikristo kuonyesha upendo na huruma kwa wote". Ulaya inashuhudia mzozo wa uhamiaji huku mamia ya watu kutoka Afrika na Mashariki ya Kati wakiwasili huko takribani kila siku.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amekutana na wakimbizi na watu maskini leo Jumamosi katika kanisa la St. Elizabeth, kanisa la matofali meupe mjini Budapest katika siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu.

St. Elizabeth alikuwa binti mfalme wa Hungary aliyeukana utajiri wake ili kujitolea maisha yake kwa watu maskini.

Papa Francis alitumia fursa hiyo kuwakumbusha Waamini wajibu wao wa Kikristo kuonyesha upendo na huruma kwa wote.

Ulaya inashuhudia mzozo wa uhamiaji huku mamia ya watu kutoka Afrika na Mashariki ya Kati wakiwasili huko takribani kila siku.

Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban amesema kwamba uhamiaji unatishia kuchukua nafasi ya utamaduni wa Kikristo barani Ulaya.

Watu wa Ulaya hawajawahi kuwa wenye hisani au kuwapokea wahamiaji hawa, lakini wamekuwa wakiwakubali zaidi Wa-ukraine waliokimbia makazi yao baada ya uvamizi wa Russia.

Papa Francis anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa vijana leo Jumamosi katika uwanja wa michezo.

Siku ya Jumapili ataongoza misa ya umma katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Pázmány Péter mjini Budapest.

XS
SM
MD
LG