Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 14, 2024 Local time: 00:41

Papa Francis aelezea kusikitishwa na idadi kubwa ya wahamiaji wanaofia kwenye bahari ya Mediterranean


Mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis
Mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis

Mkuu wa kanisa katoliki Papa Francis amesema Jumapili kwamba idadi ya wahamiaji wanaofia kwenye bahari ya Mediterranean ni ”jeraha la wazi”, kwa ubinadamu  baada ya wiki nzima iliyogubikwa na mfululizo wa ajali za boti.

Katika ibada ya kila wiki ya Angelus, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 86 aliwaombea watu 41 walioripotiwa kupotea Jumatano na wenzao wanne walionusurika na kupelekwa kwenye kisiwa cha Italy cha Lamepdusa.

Papa alisema ni “maumivu na aibu” akikumbuka takwimu za Umoja wa Mataifa, zikionyesha kwamba zaidi ya wahamiaji 2,000 wamekufa kwenye bahari ya Mediterranean tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Wakati huo huo pia aliwapongeza wote wanaojihusisha na kuzuia ajali za boti pamoja na uokozi.

Msemaji wa shirika la UN linaloshughulikia wakimbizi, IOM mwishoni mwa wiki alisema kwamba takriban watu 2,060 wamekufa kwenye bahari ya Meditarrenean tangu mwanzo wa mwaka, wakati 1,800 miongoni mwao wakipoteza maisha katikati ya bahari hiyo kati ya Afrika kaskazini kuelekea Italy na malta.

Forum

XS
SM
MD
LG