Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 22:46

Papa Benedict ajiuzulu


Pope
Papa Benedict wa 16 ameshangaza dunia Jumatatu alipotangaza anajiuzulu ifikapo februari 28, na hivyo kuwa Papa wa kwanza kujiuzulu kwa takribani miaka 600 iliyopita.

Papa aliwashangaza viongozi wa juu wa kanisa alipokutana nao huko Vatican alikotangaza uwamuzi wake. Katika taarifa yake amesema “nilitafakari kwa kina juu ya uamuzi huo.”

Benedict alisema anajiuzulu kwa sababu nguvu zake zimepunguwa sana katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita “kufikia kiwango ambacho ilibidi nitambue uwezo wangu wa kutumikia kikamilifu wadhifa wa kidini niliyokabidhiwa.”


Jopo la makadinali litakutana kumchagua Papa mpya mwishoni mwa mwezi wa Februari. .
Kujiuzulu kwa Benedict kunafungua uwezekano nadra wa kumuona Papa mpya akisimama pamoja na Papa aliyemtangulia wakati wa kutawazwa kwake.

Baba mtakatifu Benedict alizaliwa April 16 mwaka 1927 nchini Ujerumani akiwa na jina la Joseph Ratzinger. Aliwekewa mikono ya baraka kuwa kasisi mwaka 1951 na kuwa kadinali mwaka 1977. Joseph Ratzinger alichaguliwa na kuwa Papa Benedict wa 16 mwaka 2005.
XS
SM
MD
LG