Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 21:59

Papa aeleza sikitiko lake juu ya wanayotendewa wahamiaji


Papa Francis
Papa Francis

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis, ameelezea maskitiko kuhusu namna wahamiaji wanavyobaguliwa na kuhatarisha maisha yao wanapovuka bahari na majangwa wakikimbia mateso.

Akizungumza wakati wa misa ya kila wiki katika bustani ya mtakatifu Petro, Papa amewashutumu watu wanaowazuia wahamiaji kuendelea na safari zao na kuwarudisha walipotoka. Ameitaja hatua hiyo kuwa dhambi kubwa.

Francis aliwahi kusema kwamba bahari ya Mediteranean imekuwa kaburi na janga kubwa kwa watu wengi, akiongezea kwamba idadi kubwa ya watu waliofariki wangeokolewa.

Ameshukuru juhudi za wasamaria wema wanaofanya kazi kuwaokoa wahamiaji wakiwa safarini.

Papa Francis ameweka uzito mkubwa swala la uhamiaji katika uongozi wake.

Ziara yake ya kwanza nje ya Vatican kama Papa iliwa kwenye kisiwa cha Lampedusa nchini Italy ambapo mamia ya wahamiaji wamekuwa wakiwasili baada ya kutumia boti chakavu wakitokea Afrika kaskazini.

Msimamo wake kuhusu wahamiaji umekuwa kinyume na viongozi wa kisiasa wa Italy.

Waziri mkuu wa Italy Giorgia Meloni amekuwa akifanya kila juhudi kuwazuia wahamiaji kuingia Italy, na ameshirikiana na Umoja wa ulaya kusaini mikataba na Tunisia pamoja na Misri, yenye lengo la kuwazuia wahamiaji kuvuka bahari ya Mediterrania.

Forum

XS
SM
MD
LG