Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 17:10

Pande zinazozozana nchini Sudan zakubaliana kuruhusu misaada kuingia nchini


Tani za msaada wa kibinadamu kutoka kituo cha misaada cha Mfamle Salman zinapakiwa ndani ya ndege ya kijeshi ya Saudi Arabia kabla ya ndege hiyo kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Mfalme Khalid mjini Riyadh, kuelekea Port Sudan, Mei 10, 2023.
Tani za msaada wa kibinadamu kutoka kituo cha misaada cha Mfamle Salman zinapakiwa ndani ya ndege ya kijeshi ya Saudi Arabia kabla ya ndege hiyo kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Mfalme Khalid mjini Riyadh, kuelekea Port Sudan, Mei 10, 2023.

Marekani Alhamisi imeishutumu Afrika Kusini kuipa silaha Russia katika vita vyake nchini Ukraine kwenye operesheni ya siri ya siku tatu ya majeshi ya majini karibu na mji wa Cape Town mapema mwezi Disemba mwaka jana.

Wawakilishi wa jeshi na kikosi cha wanamgambo, ambao wamekuwa wakipigana kwa karibu mwezi mmoja, walisaini makubaliano mjini Jeddah, Saudi Arabia kwa “tamko la nia ya dhati kuwalinda raia wa Sudan,” alisema afisa wa Marekani anayeshiriki katika mazungumzo hayo.

Makubaliano hayo yanazitaka pande zote mbili kwa ujumla kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia nchini, kuruhusu kurejeshwa kwa umeme, maji na huduma za msingi, kuwaondoa maafisa wa usalama katika hospitali na kupanga “mazishi ya heshima” ya waliouawa katika mapigano.

Mazungumzo bado yanaendelea ili kufikia makubaliano mapya ya muda ya kuruhusu misaada, huku kukiwa pendekezo mezani la kusitisha mapigano kwa siku 10, afisa huyo wa Marekani ambaye aliomba jina lajke lihifadhiwe alisema.

XS
SM
MD
LG