Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 21:07

Pande zinazohasimiana Sudan zipo wazi kwa mashauriano ya kuleta amani

Majenerali wawili wanaohasimiana nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan (L) na Mohamed Hamdan Dagalo (R)

Volker Perthes, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan anasema pande hizo zimeteua wawakilishi kwa ajili ya mazungumzo ambayo yamependekezwa kufanyika Jeddah, Saudi Arabia, au Juba nchini Sudan Kusini ingawa alisema kuna swali la msingi iwapo kama wanaweza kufika huko na kukaa pamoja.

Pande zinazohasimiana nchini Sudan ziko wazi zaidi kwa mashauriano na zimekubali kuwa mzozo uliozuka wiki mbili zilizopita hauwezi kuendelea, afisa wa Umoja wa Mataifa ameliambia shirika la habari la Reuters siku ya Jumamosi, kuhusu uwezekano wa matumaini kidogo wakati mapigano yakiendelea.

Volker Perthes, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan anasema pande hizo zimeteua wawakilishi kwa ajili ya mazungumzo ambayo yamependekezwa kufanyika Jeddah, Saudi Arabia, au Juba nchini Sudan Kusini ingawa alisema kuna swali la msingi iwapo kama wanaweza kufika huko na kukaa pamoja.

Amesema hakuna muda maalum uliowekwa kwa ajili ya mazungumzo. Matarajio ya mashauriano kati ya viongozi wa pande mbili hadi sasa yameonekana kuwa yenye giza. Siku ya Ijumaa, kiongozi wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alisema katika mahojiano kwamba kamwe hatokaa na kiongozi wa waasi wa RSF akimaanisha Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo ambaye alisema atazungumza tu baada ya jeshi kusitisha uhasama.

Mamia ya watu wameuawa tangu Aprili 15 wakati mapambano ya muda mrefu ya kuwania madaraka kati ya jeshi na vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) walipoingia katika mzozo.

XS
SM
MD
LG