Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:21

Pande zinazo hasimiana Libya za kubali kuunda serikali ya umoja


Awad Mohammed Abdul-Sadiq (L), the first deputy head of the Tripoli-based General National Congress (GNC), and Ibrahim Fethi Amish from the internationally recognised House of Representatives sign documents after reaching an agreement on ending the politi
Awad Mohammed Abdul-Sadiq (L), the first deputy head of the Tripoli-based General National Congress (GNC), and Ibrahim Fethi Amish from the internationally recognised House of Representatives sign documents after reaching an agreement on ending the politi

Pande zinazo hasimiana nchini Libya zimekubaliana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa wakitumaini kumaliza mapigano na ghasia ambazo zimelikumba taifa hilo tangu kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa muda mrefu Moammar Gadhafi mwaka 2011.

Umoja wa Mataifa uliongoza makubaliano kwenye mkutano katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, lakini bado haijawa wazi kama itaweza kupata msaada mkubwa ili kumaliza umwagaji damu huko Libya.

Hakukuwa na majibu ya moja kwa moja kutoka makundi mawili ya nchi hiyo ambayo serikali inayotambulika kimataifa inayoendesha kazi zake kutoka mji wa Tobruk, mashariki mwa Libya na serikali inayoungwa mkono wa kundi la ki-islam linaloendesha shughuli zake katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Mkuu wa masuala ya nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini mara moja alitoa pongezi rasmi kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Mkataba wa kushirikiana madaraka umefikiwa wakati ambapo wanamgambo wa kundi la Islamic State wanapata nafasi mpya ya kuingia Libya kwa lengo la kudhibiti viwanda vya mafuta, chanzo kikuu cha utajiri wa Libya.

XS
SM
MD
LG