Pakistan na Afghanistan ndizo nchi mbili pekee duniani ambapo polio inaendelea kutishia afya na ustawi wa watoto.
Polio huathiri mfumo wa neva wa watoto na hatimaye kusababisha kupooza.
Waziri Mkuu Shahbaz Sharif, alizindua kampeni ya nchi nzima kwa kutoa matone ya polio kwa watoto katika mji mkuu, Islamabad, akisema Pakistan kwa bahati mbaya ni miongoni mwa nchi chache ambazo bado zinakabiliwa na ugonjwa huo.
Visa 20 viliripotiwa katika eneo la Waziristan Kaskazini mwaka jana, ingawa ugonjwa huo ulidhibitiwa kwa watoto wengine kupitia chanjo, Sharif alisema.
Takriban watoto milioni 44 katika wilaya 156 watapatiwa chanjo
Facebook Forum